runners runners runners runners runners runners runners


Karibu kwenye ukarasa wa mtandao wa Kushindia Dhahabu! Ukarasa huu ukawekwa kwa ajili ya kuwasiliana na washabiki wa michezo ya Jumuiya ya Madola kuhusu habari njema za Yesu Kristo na wokovu ambao anautoa kwa ajili ya ulimwengu. Michezo ya Jumuiya ya Madola ni tukio linalalowakaribisha wachezaji kutoka katika nchi 54 za Jumuiya – ni tukio mojawapo katika ya matukio makuu duniani kwa mashindano ya michezo. Kushindia medali ya dhahabu katika michezo ya Jumuiya ya Madola ni jambo kuu sana kwa mwanadamu yeyote. Hata hivyo, lililo la thamani zaidi kuliko medali ya dhahabu ni uhai wenyewe. Uhai ndiyo wa thamani sana kuliko vyote tulivyo navyo. Yesu Kristo anatoa uhai wa milele na inafaa sana kuishindia zawadi hii.

Biblia inatuambia kwamba tuliumbwa na Mungu.  Inasistiza kwamba Mungu ndiye anayetupa uhai na kutuwezesha kuishi.  Sisi tuliumbwa na Mungu ambaye anatupenda naye anataka tuwe na kusudi katika maisha yetu – hatukuwepo kwa bahati za ki-biolojia tu (Soma Zaburi 139).  Kwa sababu hii, tunawajibika mbele ya Mungu kimaadili, naye ana haki kutegemea kwamba tutatii mapenzi yake. Kwa masikitiko, wanadamu wa kwanza walikataa kumtii Mungu nao walivunja amri yake kwa makusudi (Soma Mwanzo 3). Matokeo yake yalikuwa makuu!  Tukio hili la uasi – au kama Biblia inavyosema, dhambi – liliharibu uhusiano wa pekee waliokuwa nao kwa Mungu.

Lakini si tukio la historia tu. Wazazi wetu wa kwanza walituathiri kutokana na walivyofanya. Kila mwanadamu anaye tabia hii ya uasi kama wanadamu wa kwanza; sisi sote tunafuata tamaa zetu badala ya kuishi maisha ya kumtii Mungu.  Sisi sote tunatenda dhambi.  Biblia inasema kwamba “Wote wametenda dhambi (kufanya makosa) na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23).

Hali hii ni maafa ya mwisho kwa wanadamu! Mungu anatupenda tuwe katika uhusiano na Yeye.  Anataka kutulinda na kututia moyo kama vile baba yeyote afanyavyo kwa watoto wake.  Lakini, dhambi huwa inamtenga Mungu na sisi ili kufanya uhusiano wa namna hii kuwa haiwezikani kabisa! Je, tunayo matumaini gani sasa ikiwa kweli tumetengwa na Mtoaji wa uhai?  Jibu la kweli ni – hakuna!  Kila mmoja wetu atakufa kimwili, na baada ya kifo tutahukumiwa na Mungu kwa makosa yote tuliyoyafanya.

Ndiyo, ni hali ya kutisha kwa kweli!  Walakini kuna habari njema.  Mungu anatupenda.  Anatupenda kwa maana alitoa mwanae duniani ili atuokoe (Yohana 3:16). Yesu alizaliwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita katika nchi ya Israeli.  Akaishi maisha ya ajabu katika ukamilifu, kwa kujali watu na kutenda mema.  Akawaponya wagonjwa na kuwapa vipofu kuona tena.  Akawalisha walio na njaa na kuwapa matumaini walioonewa. Miujiza yake ilithibitisha kwamba kweli alikuwa Mungu pamoja nasi katika umbo la kibinadamu.  Alipofundisha kweli juu ya Mungu na njia zake akaja kupingwa na wengi ambao hawakutaka kusikia habari hizi njema. 

Adui zake walipanga akamatwe na kusulibiwa msalabani, lakini haya yote yalikuwa sehemu ya mpango wa Mungu.  Yesu alikufa ili apokee hukumu kwa ajili ya dhambi zetu.  Mungu ambaye ndiye Mhukumu wa kila mmoja, alimhukumu Yesu kwa ajili ya makosa yetu yote.  Yesu kwa hiari yake kabisa alikubali hukumu hii kwa sababu anatupenda naye anataka tuufurahie uhusiano mpya na Mungu. Baada ya siku tatu Yesu alifufuka kutoka katika wafu, si kwa kutushawishi kuwa alikuwa nani jinsi alivyokuwa amedai, bali kutupatia msamaha wa dhambi na kutupa uzima au uhai wa milele.   

Zawadi kuu ambayo ni bora kulika zawadi zote ndiyo uzima wa milele, nao unapatikana kwa yeyote anayeomba.  Yesu anataka kutupa kiwango cha uhai ambao hauwezi kulinganishwa.  Anataka kuondoa hatia na aibu yetu na kutuwezesha kufanyika kuwa watu wa familia yake Mungu.  Tunaweza kumjua Mungu kama Baba na kupokea uhai anautoa, uzima wa milele, hata baada ya kifo cha mwili. 

Inawezekana kabisa kwamba hutapata kusimama katika jukwaa la ushindi katika michezo ya Jumuiya ya  Madola ili upokee medali ya dhahabu, lakini sasa unaweza kuwa na kitu kingine kilicho bora. Unaweza kuwa na msamaha mkamilifu wa dhambi zako zote na uzima wa milele – uhakika wa kukaa na Mungu milele mbinguni.  Kama utapenda kujua zaidi kuhusu uzima huu, tafadhali tunaomba uwasiliane kwa njia ya posta au barua pepe:

Stephen McQuoid
GLO Centre
78 Muir Street
MOTHERWELL
ML1 1BN

Au barua pepe kwa: smcquoid@glo-europe.org